Posts

Dhahabu ya Vumbi la Vikole (Gold Dust)

UVUMI KUHUSU DHAHABU

Image
Dhahabu iliyochomwa. Hivi umewahi kujiuliza kwa nini uchimbaji wa Dhahabu na madini mengine ya thamani kama Vito vya thamani (Almasi, tanzanite, yakuti samawi, zumaridi n.k) yanahusishwa sana Imani za kishirikiana!?  Kwa mfano kwenye dhahabu kuna dhana zifuatazo: ✓kuongeza/kukuza sampuli ya kwenye mtemba au ya rudio, ✓kutengeneza shimo,  ✓(gold rush) mfumuko wa ydhababu za kutengeneza, ✓kulinda sampuli n.k ✓ Pia kuna migodi wanawake hawaruhusiwi kuingia wala kusogelea!! ✓ Pia kuna wanaomini ukiwa na rudio linalosoma vizuri Sana kwenye sample unapaswa kulifunika kwa turubai kuweka uzio usio onyesha ndani la sivyo  ✓ Kuna wenye wa kuangalia na kushusha sample Yako kwa macho Yao!!! Kama wewe ni Mchimbaji au mdau wa sekta ya madini tupe uzoefu wako kwenye hii mada na kama unadhani hii mitizamo ina ukweli wowote!!  #dhahabu #gold #siri #fumbo #imani #uwekezaji #mila #tamaduni #hisia #mtazamo #tabia #sayansi #tanzania  

Uwekezaji katika Mgodi wa Dhahabu

Image
Fursa ya Kuwekeza kwenye mgodi mdogo wa dhahabu uliopo eneo la Mapogoro katika kata ya chokaa wilaya ya Chunya, mkoa wa Mbeya.  Sampuli ya mwamba inasoma kati ya 2.5g/t mpaka 3.5g/t. Mwamba una upana wa koleo moja na hivyo, upatikanaji wa mawe ya kusaga sio changamoto.  Mmiliki wa Mgodi ambaye ni mmiliki wa leseni ndogo ya uchimbaji anavifaa vyote vya muhimu kwa wachimbaji wadogo kama compressor, mono ya kuvutia maji, digger kwa ajili ya kuchorongea, karasha kwa ajili ya kusagia mawe n.k  Kiasi kinachohitajika kwa ajili ya kazi hii ni TSH. 5,000,0000/- ambacho kitatumika kwa ajili uendeshaji wa kazi kwa ajili ya kununua vilipuzi, mafuta kwa ajili ya kusagia mawe, chakula na mishahara ya wafanyakazi.  Picha hii inanyosha mtemba unatumika kuoshea mwamba wa dhahabu Malengo ni kuchimba na kusaga dumu 1200 kwa mwezi na awamu ya kwanza itafanyika kwa kipindi cha miezi 2 na wiki 3, ambapo miezi 2 itakuwa ni kuchimba na kusaga mawe na wiki tatu za mwisho ni kwa ajili ya uche...

Mradi Uliokamilika

Image
  Udhamini Unahitajika - Mradi wa Kuchenjua Rudio katika kata ya Makongolosi   Hili rudio (Tailings) lipo eneo linaitwa Ujerumani katika kata ndogo ya Mji wa Makongolosi. Maelezo ya Mradi  > Ukubwa wa rudio ni kati tani 120 mpaka 130.  > Sampuli ya  Rudio (Tailings) ni 2.72ppm.  > Umbali wa kati ya rudio na plant ni Nusu kilomita.  > Kiwanda cha kuozeshea (VAT Leaching Plant) ina tanki 5 zenye uwezo wa kubeba tani 50 kila moja, kwa hiyo mzigo wote unatarajiwa kuzungushwa kwenye mzuunguko mmoja. Hii inaaminisha mradi huu hautachukua zaidi ya wiki tatu kuanzia kuanza mpaka kukamilika.  > Matarajio ya mradi huu utazalisha kati ya gram 200 mpaka 250 za dhahabu.  Kiwango cha fedha kinachohitajika kwa mradi huu ni TZS. 6,000,000/-. Yoyote anaweza kudhamini mradi huu hata kama sio dealer wa dhahabu.  Wasiliana nasi kwa maelezo zaidi na kama ungependa kudhamini mradi huu. Unaweza kutupigia katika namba hizi: 0713332005 i...

Fedha kama Pesa.

Image
  Madini ya fedha (Silver) ni mojawapo ya madini ambatano yanayoambatana na dhahabu. Metali fedha zinaweza kutumika kwa matumizi mbalimbali kama: 1. Malighafi ya viwandani kwa aili ya kutengeneza nyaya, sakiti za kieletroniki, etc. 2. Kutengeneza urembo na mapambo mbalimbali kama hereni, pete, mifuku, saa n.k 3. Vyombo vya jikoni kama uma, vikombe, saani, bakuli n.k 4. Kutengeneza sarafu 5. Kama malighafi pesa ambapo hutuzwa katika taasisi za kifedha kama dhamana na mhusika kuchukua kiasi cha fedha kinachoshabiana na thamani husika kama mkopo.  Kiasi kikubwa cha madini fedha kinachochimbwa duniani au kupatikana wakati wa kusafisha dhahabu hutumika kwa matumizi haya matano kama yalivyoorodheshwa hapo juu ambapo asilimia kubwa hutumiwa kama malighafi pesa.  Mfumo wa kutumia madini ya thamani ambayo ni dhahabu, fedha na platinamu kama pesa au mali zinazokubaliwa kama pesa katika taasasi za kifedha na mabenki unaweza kuleta tija kubwa sana katika uchumi wetu na kuhakikisha th...

"Kucheki" - Kuangalia Sampuli

Image
Kuangalia Sampuli kwa kutumia Koleo.  Hili neno linatotumiwa na wachoji au wachimbaji wadogo kuelezea namna kuangalia Mwamba kama una Dhahabu ya Kukamatisha. Baada ya mwamba unaosemekana kuwa una dhahabu kuchimbwa! Wachimbaji husaga dumu kadha za mawe na kisha wanatumia koleo kupembua unga wa mawe yaliyosagwa ili kuona kama Kuna dhahabu huru (free gold) inavyoonekana kwa macho.  Ikiwa unga uliosagwa utaonyesha kuna mzigo (dhahabu) baada ya kuangalia sampuli kwa kutumia njia hii, basi matarajio ya kupata Dhahabu ya kukamatisha yanakuwa makubwa na kama Mwamba ni mkubwa kwa maana ya upana na urefu hiyo inaongeza uhakika wa shughuli za karashani kujiendesha na kukuza mlima wa rudio kwa haraka. Kama hakuna Dhahabu ya Kukamatisha, uendeshaji wa karasha unaweza kusuasua kwani kila wiki lazima pesa ya mafuta, chakula na oil itoke. Kiasi cha dhahabu ya kukamatisha kwa mwezi kwa wakati wa kiangazi kinaweza kufika 4 kilo kwa siku ndani ya wilaya moja kwa wilaya zenye shughuli kubwa za uc...

Namna ya Kuchukua Sampuli za Rudio kwa kutumia Bomba la chuma

Image
  Njia hii inarahisisha zoezi zima la kuchukua sampuli za Udongo kwani unaweza kuchukua sampuli nyingi kwa muda mfupi. Ila jambo la muhimu zaidi ni kwamba ubora wa sampuli ni mkubwa zaidi ukilinganisha na uchukuaji wa kutumia koleo. Changamoto inakuwa pale unapokutana na rudio lililokaa muda mrefu, linakuwa gumu sanna na zoezi la kuchukua sampuli linachukua muda mrefu. Udongo uliobebwa kutoka kwenye mashimo ya sample huchangangwa vizuri kwa pamoja ili kupata sampuli inayowakilisha vema mzigo Mzima. Namna ya Kuchukua sample kwa kutumia bomba Njia hii inarahisisha zoezi zima la kuchukua sampuli za Udongo kwani unaweza kuchukua sampuli nyingi kwa muda mfupi. Ila jambo la muhimu zaidi ni kwamba ubora wa sampuli ni mkubwa zaidi ukilinganisha na uchukuaji wa kutumia koleo. Changamoto inakuwa pale unapokutana na rudio lililokaa muda mrefu, linakuwa gumu sanna na zoezi la kuchukua sampuli linachukua muda mrefu. Udongo uliobebwa kutoka kwenye mashimo ya sample huchangangwa vizuri kwa pamoja...

Namna ya Kuchukua Sampuli za Udongo wa Dhahabu.

Image
Zipo namna kadha za kuchukua sampuli za Udongo kwa ajili ya kujua kiwango cha dhahabu kilichopo kwenye udongo husika. Namna ya kwanza ni kuchimba shimo kwa kutumia koleo, kiasi cha urefu wa mita1 au zaidi na kuchukua kiasi kidogo cha udongo kutoka kwenye ukuta wa shimo, pande zote za shimo. Idadi ya mashimo itategemeana na ukubwa wa rudio (kifusi cha udongo wenye dhahabu). Kifusi kikiwa kikubwa basi mashimo yanapaswa kuwa mengi ili kukupa sampuli inayowakilisha kwa kiasi kikubwa kiwango halisi cha dhahabu kilichopo. Uchukuaji wa sampuli kwenye rudio kwa kutumia koleo.   Kiasi kidogo cha udongo huchotwa kwenye kila ukuta wa shimo na kisha huchanganywa pamoja kupata sampuli ya ujumla. Kulingana na bajeti ya mhusika unaweza kuigawanya sampuli yako mara mbili (duplicate sample) na kurudia kipima mara ya pili baada ya majibu ya sampuli ya awali ili kujiridhisha ufanisi wa maabara iliyopima lakini pia hupima ubora sampuli zako. Hii ndio namna ya kuchukua sampuli ya rudio kwa kutumia mkon...