Namna ya Kuchukua Sampuli za Udongo wa Dhahabu.
Zipo namna kadha za kuchukua sampuli za Udongo kwa ajili ya kujua kiwango cha dhahabu kilichopo kwenye udongo husika. Namna ya kwanza ni kuchimba shimo kwa kutumia koleo, kiasi cha urefu wa mita1 au zaidi na kuchukua kiasi kidogo cha udongo kutoka kwenye ukuta wa shimo, pande zote za shimo. Idadi ya mashimo itategemeana na ukubwa wa rudio (kifusi cha udongo wenye dhahabu). Kifusi kikiwa kikubwa basi mashimo yanapaswa kuwa mengi ili kukupa sampuli inayowakilisha kwa kiasi kikubwa kiwango halisi cha dhahabu kilichopo.
Majibu ya sampuli yanawakilishwa katika mfumo wa gramu kwa tani!(g/t) au sehemu Moja kwa sehemu milioni Moja (part per million-ppm). Kwa mfano: 2g/t (2ppm) inamaanisha kwenye kila tani moja ya kifusi cha udongo kuna gramu mbili za dhababu. Kulingana na majibu uliyopata utapaswa kufanya mahesabu na kukadiria kiasi Gani dhahabu rudio la linapaswa kukuzalishia. Tutazungumzia kwa undani kipande hiki cha uwasilishwaji wa vipimo vya dhahabu kwenye rudio, mtemba na carbon katika makala zinazofuata.
Kama una swali lolote kuhusiana na namna ya Kuchukua Sampuli za Udongo wenye dhahabu tafadhali liweke kwenye maoni hapo chini. Pia kama umependa makala hii like na fuata ukarasa wetu na washirikishe wengine pia.

Comments
Post a Comment