Mradi wa Shinyampwaga

Huu ni mradi wa Uchimbaji dhahabu katika eneo ambalo tayari kazi ya uchimbaji imekuwa ikifanyika kwa miaka kadhaa. Bw. I.M ni mchimbaji mdogo ambaye ni mmiliki wa leseni halali ya kuchimba madini ya dhahabu katika eneo linaloitwa Shinyampwaga, kijiji cha Shoga, kata ya Sangambi, wilaya ya Chunya, mkoa wa Mbeya. Anahitaji uwezekezaji wa jumla ya shilingi za kitanzania Milioni tano tu. (TZS. 5,000,000/-) kwa ajili ya kuendesha shughuli zake za uchimbaji katika leseni yake ya uchimbaji. 

Pia Bw. I.M ni anamiliki vifaa vifuatavyo kwa ajili ya kuendesha kazi zake za uchimbaji: air compressor, jack hammer kwa ajili ya kuchorongea na karasha kwa ajili ya kusagia mawe. 



Matumizi ya fedha husika yatakuwa kama ifuatavyo:

1. Vilipuzi kwa ajili ya mwamba: Futa Boski 3, Cordtex roller 3, Pin box 3 - TZS. 1.68Mil

2. Diesel lita 150 - TZS. 0.48Mil

3. Petroli lita 30 - TZS. 0.165Mil

4. Usafiri wafanyakazi wapya - TZS. 0.54Mil

5. Deni la Malipo ya wafanyakazi waliopo - TZS. 1.5Mil

6. Dharura na Mengineyo: TZS. 0.635Mil

Maelezo kitaalamu kuhusu Mradi huu: 

1. Upana wa Mwamba - 15cm mpaka 40cm.

2. Sampuli ya udongo uliosagwa kutoka kwenye mwamba husika; 8g/t - 12g/t.

3. Kipindi cha Uzalishaji - April - October 2023.

4. Tani zinazotarajiwa kuchimbwa: Tani 120 - 170. 

5. Kiwango cha Dhahabu kitakachopatikana - 1kg mpaka 1.4kg.

Mwekezaji atarudishiwa fedha yake yote aliyotoa mara baada ya mlima wa rudio kuozeshwa kwenye VAT Leaching plant mwezi november mwaka huu (2023) na kupata asilimia 10 ya dhahabu yote iliyopatikana mara baada ya kutoa gharama za uendeshaji. 

Kwa maelezo zaidi tafadhali wasiliana nasi katika namba zifuatazo 0713332005 au kwa anuani ya barua pepe: aimborametals@gmail.com, pia unaweza kuja moja kwa moja kwenye ofisi zetu zilizoko Chunya mjini, barabara ya Itigi, ghorofa ya Mwembe, sakafu ya tatu,  kwa ajili ya kwenda kukagua eneo hili ambapo mradi huu unapatikana. 

Comments

  1. Habari, inamaanisha kazi itakua inajiendesha baada ya kupatiwa huo mtaji? Je dhahabu za kukamatisha ni kiasi gani kwa dumu (mfuko)

    ReplyDelete
  2. dhahabu ya kukamatisha inapatikana kuanzia 0.1gramu kwa dumu mpaka 0.3gramu kwa dumu.

    ReplyDelete

Post a Comment

Mradi wa Shinyampwaga

UVUMI KUHUSU DHAHABU

Dhahabu ya Vumbi la Vikole (Gold Dust)

Dhahabu ya Kukamatisha (Gold Amalgam)