Dhahabu ya Kukamatisha (Gold Amalgam)

Hii ni Dhahabu inayopatikana baada ya mwamba wenye Dhahabu kupondwa pondwa na kusagwa, kisha mchanga unaopatikana kuoshwa juu ya mtemba (mbao iliyotandikwa gunia iliyolazwa kimshazari) na ili kupembua Dhahabu-huru iliyokobolewa kwa njia upondaji na usagaji wa jiwe. 



Picha hii inanyosha dhahabu ya kukamatisha ambayo ni hizo gololi kubwa zinazoonekana na vumbi la dhahabu linalotokana kuseka mchanga pembezoni mwa mito, mitaro na makorongo. 


Kwa kuwa dhahabu ni moja ya metali nzito sana, hubaki katika matundu ya gunia lililotandikwa kwenye mtemba, na baadae hukung'utwa ndani ya pipa la maji na kisha mchanga uliopatikana huchanganywa na madini ya zebaki (mercury) ambayo huikamata dhahabu iliyopo katika mchanga. Sehemu ya mchakato huu wa Kukamatisha dhahabu huitwa "kupiga yuku" na inahitaji uzoefu na ujuzi mzuri ili kukamatisha dhahabu kwa asilimia kubwa. 

Mchanganyo wa Dhahabu na mercury unaopatikana baada ya kupiga yuku huchunjwa katika kitambaa na kisha gololi zilizopatikana huchomwa katika jiko la mkaa na kupata dhahabu mbichi kama inavyoonekana kwenye picha hapo juu. Dhahabu mbichi hiyo ikifika sokoni huchomwa (huyeyushwa) kwa kutumia gesi na kuunganishwa kuwa mche yabisi.



Hizo gololi ambazo zinaonyesha kama namna ya kufubaa ndizo zimetokana na mchakato wa kukamatisha dhahabu kwa kutumia zebaki. 

Comments

Mradi wa Shinyampwaga

UVUMI KUHUSU DHAHABU

Dhahabu ya Vumbi la Vikole (Gold Dust)