Karasha - Pembejeo ya Lazima kwa Mchimbaji Mdogo




Hiki ni mashine ya kusaga mawe. Inatengenezwa hapa nchini karibia kila mahali kwenye maeneo ya uchimbaji wa Dhahabu. Inajumuuisha sehemu tatu kuu, Engine kwa ajili ya kuzalisha nguvu ya kuendeshea, Gearbox na propeller yake kwa ajili ya kusafirisha nishati kutoka kwenye engine kwenda kwenye mtungi. Sehemu ya tatu ni Mtungi ambao umebeba gololi za chuma zinazoponda mawe yenye dhahabu. 



Video: inaonyesha usagaji wa mawe ukiendelea kwa kutumia karasha linalotengenezwa na wenyeji lenye uwezo wa kusaga mawe yenye uzito wa kilo mia mbili (200kg) kwa lisaa limoja.

Mitungi mingi huwa inauwezo wa kusaga kilo 200 mpaka 250 za mawe ya mwamba wenye dhahabu kwa dakika 45. Kila Mtungi lazima uwe na gololi zisizo pungua 300. Ukubwa wa gololi hutofautiana lakini wengi hupendelea gololi zenye unene(kipenyo) cha milimita arobaini (40mm), za 60mm, za 80mm na 110 au 120Mm). Gololi nyingi huwa kati ya 60mm na 80mm. Wingi wa gololi na uwiano sahihi kulingana na ukubwa wa kipenyo cha gololi itasaidia usagaji na uivishaji haraka wa unga wenye dhahabu. Makarasha mengi yanaweza kufanya Kazi kwa masaa 10 kwa shifti Moja, mengine yanafanya kazi usiku mchana. 

Gharama ya kutengeza karasha moja inatofautiana kati ya eneo Moja na lingine, pia kulingana ukubwa wa mtungi na aina ya engine itakayotumika. Makarasha mengi yanaanzia TZS. 8Mil kwenda mbele kwa makarasha mapya na bei ya used ni kulingana na muuzaji. Uwekezaji wa kwenye karasha ni muhimu sana na tutatazama faida na hasara zake katika episode zinazofuata.

Comments

Mradi wa Shinyampwaga

UVUMI KUHUSU DHAHABU

Dhahabu ya Vumbi la Vikole (Gold Dust)

Dhahabu ya Kukamatisha (Gold Amalgam)