Uchimbuaji wa Mwamba wenye Dhahabu.
Hii ni sehemu ya kwanza na muhimu sana katika mnyororo wa thamani sekta ya uchimbaji. Inahusisha hatua muhimu sana kama; survey (ili kugundua mwamba wenye Mali) hatua ambayo hufanywa na wanajiolojia wa kienyeji ambao wengi wamejifunza kupitia uzoefu wa miaka kadha kwenye shughuli za uchimbaji katika maeneo husika.
Mwamba wa dhahabu unaochimbwa maeneo ya kwa Mjerumani kata ya Matundasi, wilaya ya Chunya
Hatua ya pili ni utoaji wa mawe kutoka kwenye shimo husika na kuangalia sampuli ya jiwe kwa kutumia koleo (au bakuli ndogo ya chuma) kujua kama kuna dhahabu huru (free gold) inavyoonekana kwa macho!
Hatua ya tatu ni kuosha unga uliosagwa kwa kutumia tekinolojia ya mtemba na kukamatisha dhahabu kwa kutumia zebaki (kipimo kinachotumika kupimia kiasi cha unga wa mawe yaliyosagwa ni mifuko ya viroba ya kilo 20 ambayo hufafanishwa na dumu moja la lita 20- Yale madumu ya rangi ya njano). Wachimbaji huwa makini kuosha dumu kadha za unga wa mawe, halafu hulinganisha idadi ya gramu za Dhahabu iliyopatikana na jumla ya dumu zilizosagwa na kuoshwa. Dumu Moja likitoa kuanzia 0.1gram ya Dhahabu basi kuna uwezakano mkubwa shughuli za karashani zikajiendesha zenyewe bila kuhitaji nyongeza ya mara kwa mara ya mtaji wa uendeshaji.
Kwa kifupi hivi ndivyo kifundo cha kwanza cha mnyororo wa thamani kinavyokuwa. Kwa mwenye maswali au maoni tafadhali weka hapo chini kwenye comment na tutapenda kukujibu maswali yenu au kusikia maoni yenu.
Rundo la mawe yasiyochimbwa tayari kwa ajili ya kusagwa.
Hatua ya Nne: Ni upimaji wa rudio (udongo uliooshwa na kuchenjuliwa dhahabu huru kwa kutumia zebaki) ili kujua ni kiasi gani cha Dhahabu kipo au kimebaki. Upimaji hufanyika katika maaraba za miamba na majibu huchukua mpaka saa4 kukamilika. Majibu haya yanampa mchimbaji hamasa ya kuendelea kama ni mazuri kuanzia 1g/T (1gram kwa tani Moja ya udongo) au yanamkata hamasa ya kuendelea kama yapo chini ya 1g/T. Pia kama upana wa Mwamba ni chini ya sentimeta 20 basi sampuli ndogo kama 1g/T inakuwa haina tija kuichimba isipokuwa kuna uwezakano wa Mwamba kuendelea kutanuka kwa kadiri shimo litakavyozidi kwenda chini.
Mlima wa rudio(mchanga wa dhahabu) unaosubiri kuchenjuliwa
Kwa kifupi hivi ndivyo kifundo cha kwanza cha mnyororo wa thamani kinavyokuwa. Kwa mwenye maswali au maoni tafadhali weka hapo chini kwenye comment na tutapenda kukujibu maswali yenu au kusikia maoni yenu.




Comments
Post a Comment