"Kucheki" - Kuangalia Sampuli

Kuangalia Sampuli kwa kutumia Koleo. 

Hili neno linatotumiwa na wachoji au wachimbaji wadogo kuelezea namna kuangalia Mwamba kama una Dhahabu ya Kukamatisha. Baada ya mwamba unaosemekana kuwa una dhahabu kuchimbwa! Wachimbaji husaga dumu kadha za mawe na kisha wanatumia koleo kupembua unga wa mawe yaliyosagwa ili kuona kama Kuna dhahabu huru (free gold) inavyoonekana kwa macho. 

Ikiwa unga uliosagwa utaonyesha kuna mzigo (dhahabu) baada ya kuangalia sampuli kwa kutumia njia hii, basi matarajio ya kupata Dhahabu ya kukamatisha yanakuwa makubwa na kama Mwamba ni mkubwa kwa maana ya upana na urefu hiyo inaongeza uhakika wa shughuli za karashani kujiendesha na kukuza mlima wa rudio kwa haraka. Kama hakuna Dhahabu ya Kukamatisha, uendeshaji wa karasha unaweza kusuasua kwani kila wiki lazima pesa ya mafuta, chakula na oil itoke.

Kiasi cha dhahabu ya kukamatisha kwa mwezi kwa wakati wa kiangazi kinaweza kufika 4 kilo kwa siku ndani ya wilaya moja kwa wilaya zenye shughuli kubwa za uchimbaji. Kwa hiyo dhahabu ya kukamatisha inachangia kwa kiasi kikubwa sana sekta nzima ya madini ya metali.

Unaweza kutazama namna kupiga sample au chabo kwa kutumia koleo, kwa kubofya link hapo chini na kutazama video hii.

@aimborametals




Comments

Mradi wa Shinyampwaga

UVUMI KUHUSU DHAHABU

Dhahabu ya Vumbi la Vikole (Gold Dust)

Dhahabu ya Kukamatisha (Gold Amalgam)