Fedha kama Pesa.

 


Madini ya fedha (Silver) ni mojawapo ya madini ambatano yanayoambatana na dhahabu. Metali fedha zinaweza kutumika kwa matumizi mbalimbali kama:

1. Malighafi ya viwandani kwa aili ya kutengeneza nyaya, sakiti za kieletroniki, etc.

2. Kutengeneza urembo na mapambo mbalimbali kama hereni, pete, mifuku, saa n.k

3. Vyombo vya jikoni kama uma, vikombe, saani, bakuli n.k

4. Kutengeneza sarafu

5. Kama malighafi pesa ambapo hutuzwa katika taasisi za kifedha kama dhamana na mhusika kuchukua kiasi cha fedha kinachoshabiana na thamani husika kama mkopo. 



Kiasi kikubwa cha madini fedha kinachochimbwa duniani au kupatikana wakati wa kusafisha dhahabu hutumika kwa matumizi haya matano kama yalivyoorodheshwa hapo juu ambapo asilimia kubwa hutumiwa kama malighafi pesa. 

Mfumo wa kutumia madini ya thamani ambayo ni dhahabu, fedha na platinamu kama pesa au mali zinazokubaliwa kama pesa katika taasasi za kifedha na mabenki unaweza kuleta tija kubwa sana katika uchumi wetu na kuhakikisha thamani ya pesa yetu (fiat currency) inaimarika kwa namna ya kipekee sana. Metali hizi za thamani zingeweza kuuzwa na kununuliwa katika masoko yetu ya mitaji ya ndani na kufanya wa taasisi zetu za kifedha na mabenki kutunza hazina zao au mitaji yao katika mfumo wa metali za thamani na hivyo kulinda na kuimarisha thamani ya shilingi yetu. 



Thamani ya metali hizi zimekuwa zikipanda sana katika soko la dunia kwa miaka kadhaa sasa kwa mfululizo na hivyo kutunza pesa zetu katika mfumo wa metali za thamani kama madini fedha kunahakikisha thamani ya pesa yako haiathiriwi na kupanda na kushuka kwa thamani pesa au mdororo wa uchumi duniani. Kumbuka pia ukiwa na metali hizi za thamani unaweza kuuza muda wowote na kwa yeyote ndani au nje ya nchi, kwani hii ni bidhaa ambayo haina hati miliki ya nchi fulani au kampuni fulani. 

Amka leo na uanze kuwekeza katika metali za thamani kama fedha, dhahabu na platinamu. Wasiliana nasi kwa maelezo zaidi ya namna ya kufanya hivyo (0754600080), lakini weka maoni au maswali yako katika sanduku la maoni hapo chini. 

 



Comments

  1. Hii imenifungua kitu sana. Nahitaji kuelewa zaidi ni Kwa namna gani madini yanasaidia kuimarika Kwa fedha ya nchi na kuzuia isiathiriwe na anguko la uchumi kidunia. Nitapata wasaa mzuri kurudia kusoma Leo pamoja na makala zingine, nimevutiwa sana. Nitamtumia na mke wangu😆

    ReplyDelete
    Replies
    1. asante sana kwa maoni yako na tumefurahi kujua tumeweza kuchochea hamasa nzuri ndani yako kwenye mada hii! tutafanya uchambuzi kina kidogo kwenye andiko lijalo kuhusu namna madini yanavyoweza kuimarisha fedha za nchi mbalimbali zisiathiriwe na anguko la uchumi wa kidunia. Naamini tutaweza kujibu swali lako kwa kiasi fulani.

      Delete

Post a Comment

Mradi wa Shinyampwaga

UVUMI KUHUSU DHAHABU

Dhahabu ya Vumbi la Vikole (Gold Dust)

Dhahabu ya Kukamatisha (Gold Amalgam)