Fursa ya Kuwekeza kwenye mgodi mdogo wa dhahabu uliopo eneo la Mapogoro katika kata ya chokaa wilaya ya Chunya, mkoa wa Mbeya.
Sampuli ya mwamba inasoma kati ya 2.5g/t mpaka 3.5g/t. Mwamba una upana wa koleo moja na hivyo, upatikanaji wa mawe ya kusaga sio changamoto.
Mmiliki wa Mgodi ambaye ni mmiliki wa leseni ndogo ya uchimbaji anavifaa vyote vya muhimu kwa wachimbaji wadogo kama compressor, mono ya kuvutia maji, digger kwa ajili ya kuchorongea, karasha kwa ajili ya kusagia mawe n.k
Kiasi kinachohitajika kwa ajili ya kazi hii ni TSH. 5,000,0000/- ambacho kitatumika kwa ajili uendeshaji wa kazi kwa ajili ya kununua vilipuzi, mafuta kwa ajili ya kusagia mawe, chakula na mishahara ya wafanyakazi.
Picha hii inanyosha mtemba unatumika kuoshea mwamba wa dhahabu
Malengo ni kuchimba na kusaga dumu 1200 kwa mwezi na awamu ya kwanza itafanyika kwa kipindi cha miezi 2 na wiki 3, ambapo miezi 2 itakuwa ni kuchimba na kusaga mawe na wiki tatu za mwisho ni kwa ajili ya uchenjuaji. Hivyo ndani ya awamu ya kwanza ya mradi tunarajia kuzalisha dumu 2400 za mawe ambazo ni sawa na tani 200 au tanki 4 kwa lugha ya kichimbaji. Makadiro ya chini ya mradi huu ni kupata gramu 300 za dhahabu, ambapo mwekezaji atakuwa na asilimia 25% ya faida yote itakayopatikana ambayo haitakuwa chini ya 60% ya fedha yote aliyowekeza. Mwekezaji au Mdhamini atakuwa na fursa ya kuendelea kuwekeza kama atapenda mara baada ya awamu ya kwanza ya mradi kukamilika.
Picha hii inaonyesha jiwe la Mwamba
Aimbora Metals Ltd itakuwa mdhamini wa mradi huu na hivyo kiasi cha fedha kilichowekwa na mwekezaji/mdahamini kitalindwa na kusimamiwa ipasavyo na kuhakikishwa kinatumika kama ilivyopangwa na ikiwa mradi umeshindwa kuzalisha kufikia malengo na matarajio kwa sababu zozote zile za asili au za kibinadamu, kampuni ya Aimbora itawajibika kurejesha fedha yote ya mwekezaji pamoja na riba ya 5% kila mwezi kwa kipindi cha chote cha mradi ambapo pesa ya mwekezaji au mdhamini ilikuwa imetolewa.
Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kwa namba zifuatazo: 0713332005 au 0754600080.
Comments
Post a Comment