Mradi Uliokamilika

 Udhamini Unahitajika - Mradi wa Kuchenjua Rudio katika kata ya Makongolosi



 Hili rudio (Tailings) lipo eneo linaitwa Ujerumani katika kata ndogo ya Mji wa Makongolosi.

Maelezo ya Mradi 

> Ukubwa wa rudio ni kati tani 120 mpaka 130. 

> Sampuli ya  Rudio (Tailings) ni 2.72ppm. 

> Umbali wa kati ya rudio na plant ni Nusu kilomita. 

> Kiwanda cha kuozeshea (VAT Leaching Plant) ina tanki 5 zenye uwezo wa kubeba tani 50 kila moja, kwa hiyo mzigo wote unatarajiwa kuzungushwa kwenye mzuunguko mmoja. Hii inaaminisha mradi huu hautachukua zaidi ya wiki tatu kuanzia kuanza mpaka kukamilika. 

> Matarajio ya mradi huu utazalisha kati ya gram 200 mpaka 250 za dhahabu. 

Kiwango cha fedha kinachohitajika kwa mradi huu ni TZS. 6,000,000/-. Yoyote anaweza kudhamini mradi huu hata kama sio dealer wa dhahabu. Wasiliana nasi kwa maelezo zaidi na kama ungependa kudhamini mradi huu. Unaweza kutupigia katika namba hizi: 0713332005 inapatikana pia kwa njia ya whatsapp.

Mrejesho wa Mradi uliokamilika. 


Hii ni dhahabu iliyopatikana kutoka kwenye mradi huu, zaidi ya gram 220 na purity ya mzigo ilikuwa nzuri sana - kubwa 98% na ndogo 90%. Mdhamini na mdhaminiwa wote walikuwa na furaha kwa kazi nzuri tuliyoifanya na tunatarajia kufanya kazi nao tena katika siku za usoni. 



#udhamini #rudio #uwekezaji #thamani #investment #fursa #opportunity #gold #mining

Comments

  1. Huu mradi umekamilika, na mteja amepata kama tulivyofanya makadirio na kwa muda tulio mkadiria. kila jambo limekwenda sawa na bajeti tuliomwandalia mteja.

    ReplyDelete

Post a Comment

Mradi wa Shinyampwaga

UVUMI KUHUSU DHAHABU

Dhahabu ya Vumbi la Vikole (Gold Dust)

Dhahabu ya Kukamatisha (Gold Amalgam)